Serikali ya Austria kumiliki nyumba ya Hitler

Image caption Nyumba aliyozaliwa Hitler

Serikali ya Austria imesema kuwa inanuia kutwaa umiliki wa nyumba ambayo Adolf Hitler alizaliwa, ili kuizuia nyumba hiyo kuwa kituo maalum cha watu wanaounga mkono utawala wa kinazi.

Msemaji wa wizara ya usalama wa ndani amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya miaka kadhaa ya majadiliano ya jinsi ya kuzuia hisia zinazokuza utawala wa kinazi.

Kiongozi huyo wa zamani wa Ujerumani alizaliwa katika nyumba hiyo iliyoko Braunau mwezi Aprili mwaka wa 1889.

Serikali ya nchi hiyo ilikodi nyumba hiyo kutoka kwa mmiliki wake tangu mwaka wa 72 na imekuwa ikitumika kama kituo cha kuwahudumia watu walemavu.