Wakimbizi wa Palmyra warudi nyumbani

Image caption Palmyra

Mabasi yaliosheheni wakimbizi wanaorejea nyumbani, yanatarajiwa kuwasili katika mji wa kale wa Palmyra nchini Syria, takriban wiki mbili baada ya wanajeshi wa serikali kuukomboa mji huo kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Wakaazi wa eneo hilo wameruhusiwa kurejea baada ya wanajeshi wa serikali kuondoa vilipuzi vilivyokuwa vimetegwa mjini humo na wanamgambo hao wa Kiislamu.

Maelfu ya watu walikimbia mji huo baada ya wapiganaji hao wa Islamic state kuuteka Mei mwaka uliopita.

Maafisa wa serikali wanasema kuwa sehemu kubwa ya mji huo umeharibiwa, ikiwemo baadhi ya makavazi ya zamani ya kitaifa ambayo yaliorodheshwa na Umoja wa mataifa kama maeneo ya hifadhi za kale.