Aliyekuwa Spika Marekani ahusika na dhulma za kingono

Image caption Aliyekuwa Spika wa marekani Denis Hastert

Waendesha mashtaka nchini Marekani wanasema kuwa aliyekuwa spika wa bunge la wawakilishi, Denis Hastert, alikubali kulipa dola milioni tatu na nusu kisiri, ili kuficha kuhusika kwake na unyanyazaji wa kingono dhidi ya wavulana kadhaa.

Katika nyaraka zilizowasilishwa mbele ya mahakama siku ya Ijumaa, waendesha mashtaka hao wanasema fedha hizo zililipwa kwa mtu ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na minne wakati alipodhulumiwa miongo kadhaa iliyopita.

Image caption Aliyekuwa spika wa bunge la Marekani Kulia Denis Hastert akiwa na rais wa zamani Bush

Oktoba mwaka uliopita, spika huyo wa zamani alikiri kuwa alivunja sheria za benki kwa kumlipa fidia mtu mmoja ambaye hakutajwa.

Wanasema bwana Hastert ambaye ana umri wa miaka 74, aliwadhulumu kimapenzi wavulana wengine watatu wakati alipokuwa kocha wa mieleka kabla ya kujiunga na siasa. Hastert atahukumiwa baadaye mwezi huu.