Abu Sayyaf waua wanajeshi 18 Ufilipino

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wenye msimamo mkali wa kidini wa Abu Sayyaf wamewaua wanajeshi 18 Ufilipino

Jeshi la Ufilipino limekiri kuwa wanajeshi 18 wameuawa katika makabiliano makali na wapiganaji waasi wa Abu Sayyaf Kusini mwa taifa hilo.

Limeongeza kuwa wanajeshi wengine 50 walijeruhiwa wakati wa makabiliano katika kisiwa cha Basilan.

Wapiganaji watano wa kundi hilo la Waislamu wenye itikadi kali waliuawa.

Inasemekana wanajeshi walikuwa wakimlenga kamanda wa Abu Sayyaf Isinilon Hapilon, ambaye ameapa uaminifu wake kwa kundi la Islamic State.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kamanda wa Abu Sayyaf Isinilon Hapilon,ameapa uaminifu wake kwa kundi la Islamic State.

Kundi la Abu Sayyaf limetekeleza ulipuaji wa mabomu, utekaji nyara na kuwakata watu vichwa Kusini mwa Ufilipino.

Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya dola milioni 5 kwa habari zozote zitakazosaidia kumtia mbaroni Hapilon.