Waliouza maziwa ya watoto yenye sumu wanaswa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waliouza maziwa ya watoto yenye sumu wanaswa

Watu 9 wamekamatwa kwa tuhuma za kuuza maziwa ya watoto yenye sumu nchini Uchina.

Maafisa wa afya nchini Uchina wanasema wamewakamata watu hao katika kilele cha moja kati ya kashfa kadha kuhusu usalama wa wateja.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waliokamatwa ni kati ya genge ambalo lilinua maziwa ya unga kwa bei rahisi na kisha kuyaweka kwenye makopo ya chapa ghali.

Waliokamatwa ni kati ya genge ambalo lilinua maziwa ya unga kwa bei rahisi na kisha kuyaweka kwenye makopo ya chapa ghali.

Polisi mjini Shanghai wamechunguza kisa hicho tangu Septemba mwaka jana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya watu wamelalamika kuwa habari hizo zimechelewesha kutolewa.

Baadhi ya watu wamelalamika kuwa habari hizo zimechelewesha kutolewa.

Mwezi uliopita, wakuu waliwakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kuuza chanjo ghushi na zisizofaa.