Sanders amshinda bi Clinton huko Wyoming

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bernie Sanders amshinda Hillary Clinton katika jimbo la Wyoming

Bernie Sanders ameshinda kura za mchujo katika chama cha Democratic katika jimbo la Wyoming.

Seneta Sanders ameshinda majimbo saba kati ya nane yaliyobakia.

Amesema kuwa kampeni yake imeshika kasi wakati ambapo yeye na mpinzani wake mkuu Hillary Clinton wanasubiri uchaguzi mwingine wa mchujo katika jimbo maarufu kisiasa la New York, mwezi ujao.

Licha ya ushindi wake katika majimbo hayo, mshindani wake mkuu Hillary Clinton angali ana idadi kubwa zaidi ya wajumbe katika kinyanganyiro hicho cha mchujo wa kuwakilisha chama chao kungangania Urais.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Licha ya ushindi wake katika majimbo hayo, mshindani wake mkuu Hillary Clinton angali ana idadi kubwa zaidi ya wajumbe

Kwa upande wa Republican, Ted Cruz anatarajia kuendelea kumsukuma kiongozi wa sasa katika uchaguzi huo wa mchujo, Donald Trump hadi mkutano wa mwisho wa kitaifa wa chama katika Colorado.