Saudia yatoa dola bilioni 16 kujenga Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Saudia yatoa dola bilioni 16 kujenga Misri

Saudi Arabia na Misri zinaazmia kuunda hazina ya pamoja ya dola bilioni za Marekani 16 zitakazotumiwa kwa uwekezaji.

Mkataba huo ulitangazwa jijini Cairo wakati wa siku ya kwanza ya ziara ya Mfalme Salman.

Ziara hiyo ya siku tano na Mfalme huyo wa Saudi Arabia inaonekana na wachanganuzi wengi kama kuungwa mkono kwa rais Abdel-Fattah al-Sisi, ambaye anajaribu kufufua uchumi wa taifa lake.

Tayari Saudi Arabia imetoa mabilioni ya dola za msaada na uwekezaji nchini Misri.