Maharamia wateka meli ya Uturuki Nigeria

Image caption Kumekuwa na ongezeko la visa vya uharamia Afrika ya Magharibi

Maharamia katika pwani ya Nigeria wameshambulia meli ya mizigo ya Uturuki na kuwateka nyara wafanyikazi sita wa meli hiyo, katika eneo hilo ambalo limeshuhudia visa vingi vya uharamia miaka ya hivi karibuni.

Shirika la habari la Deniz lilisema kuwa wale waliotekwa nyara walikuwa ni pamoja na mhandisi ya mitambo, fundi wa umeme pamoja na muelekezi.

Meli hiyo inamiikiwa na kampuni ya Kaptanogul, ambayo ililiambia shirika hilo la habari kuwa wale waliotekwa nyara pamoja na wale waliosalia melini wote wako katika hali nzuri ya afya.

Haijulikani ni wafanyikazi wangapi walikuwa ndani ya meli hiyo, ambayo ilikuwa ilikuwa ikisafirisha kemikali wakati iliposhambuliwa, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.