Vikosi vya waasi vimerejea Juba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi nchini Sudan Kusini

Vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini vimekamilisha shughuli ya kurejea mji mkuu wa Juba, kama sehemu ya mpango wa amani uliotiwa sahihi kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda wa miaka miwili unusu.

Kikosi hicho cha wanajeshi 1370 walisafirishwa kwa ndege iliyofadhiliwa na umoja wa mataifa kwenda kwenda Juba kama inavyohitajika kwenye awamu ya kwanza ya mpango huo.

Wanatarajiwa kumhakikishia usalama kiongozi wa waasi Riek Machar, ambaye aliteuliwa kuwa makamu wa rais kwenye serikali ya mpito na ambaye anatarajiwa kuwasili Juba mwezi Ujao.

Mapigano yamewalazimu zaidi ya watu milioni 2.2 kukimbia makwao, katika taifa hiyo janga zaidi duniani tangu mwaka 2103.