Taiwan yapinga raia wake kupelekwa China

Image caption Taiwan haina uhusiano mzuri na jirani wake China

Serikali ya Taiwan imelalamika baada ya raia wake wanane kusafirishwa kwa lazima kwenda China baada ya wao kuondolewa mashtaka ya ulaghai nchini Kenya.

Taiwan imeushutumu utawala wa China kwa hatua zake ilizilinganisha na utekaji nyara.

Wanane hao ni miongoni mwa raia 23 wa Taiwan walioondolewa mashtaka ya kuwa miongoni mwa watu waliokisiwa kupanga ulaghai wa simu wakiwemo pia raia wa China.

Taiwan inasema kuwa wakati watu hao walienda kuchukua paspoti zao kutoka kwa polisi wa Kenya, walikamatwa na kuingizwa kwa ndege na maafisa wa China.

Uhusiano kati ya China na Taiwan unaendelea kuzorota wakati China ikiitaja Taiwan kama mkoa wake uliojitenga ambapo imetishia kuurejesha kwa nguvu ikiwa itahitajika.