Visa vya kujiua vimeongezeka Canada

Image caption Wataalamu wanasema kuwa umaskini na ukosefu wa matumaini maishani ndizo sababu kuu za kuongezeka kwa visa vya kujiua

Kikosi cha dharura cha kushughulikia matatizo ya kisaikolojia kimetumwa kwenda kwa jamii moja iliyotengwa nchini Canada kushughulikia kuongezeka kwa visa vya kujiua.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili katika eneo la Attawapiskat, ambapo kuna jamii ya watu 2000 Kaskazini mwa mkoa wa Ontario siku chache zinazokuja.

Viongozi wa kijamii wanasema kuwa kumekuwa na visa vya majaribio ya kijiua karibu 100 miezi sita iliyopita.

Wataalamu wanasema kuwa umaskini na ukosefu wa matumaini maishani, ndizo sababu kuu za kuongezeka kwa visa hivyo.

Waziri wa afya nchini Canada anasema kuwa serikalia imefanya mikakati kuhakikisha kuwa huduma za afya zipo ili kushugulikia hali hiyo.