Panya wailazimu Uingereza kukodisha paka

Image caption Panya wailazimu Uingereza kukodisha paka

Je unampenda paka ?

Awe ni paka wa nyumbani ama yule paka wa mwituni na wanyama wote katika jamii ya pakaa kama vile simba,ama chui, paka huvutia hisia nyingi sana kwa mwanadamu.

Video za paka ni maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii.

Image caption Je unampenda paka ?

Lakini mapenzi hayo ya paka yamefikia hatu mpya.

Amini usiamini afisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.

Image caption Afisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.

Paka huyo ambaye zamani alinusuriwa alipokuwa akizurura mitaani katika mji mkuu wa London -- alipewa jina Palmerston, jina la waziri mashuhuri wa zamani wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza na waziri mkuu karne ya kumi na tisa.

Kituo cha kuwanusuru wanyama, kimesema kwamba Palmerston, alikuwa mkakamavu na paka mwenye nguvu, ambaye haikuwa vigumu kwake kuwa na marafiki -- au maadui, katika makao hayo yake mapya katika afisi ya wizara ya nchi za kigeni.