Sheria mpya dhidi ya wanaokwepa kodi Ulaya

Image caption Sheria mpya dhidi ya wanaokwepa kodi Ulaya

Baraza kuu la mataifa ya bara Ulaya, limeorodhesha mikakati mipya hii leo ya kuzilazimisha kampuni za kimataifa kuchapisha taarifa ya kina ya faida zinazopata na ushuru wanayotozwa, katika mataifa yote 28 wanachama wa EU.

Mapendekezo hayo yatajumuisha faida ya kampuni hizo kubwa za kimataifa inayokisiwa kuwa zaidi ya Euro 750.

Mpango huo wa kutangaza faida na ushuru wazi ni njia mojawepo ya kutokomeza kabisa ufisadi na ukwepaji wa kulipa ushuru ambao ulipingwa mwaka 2014, na haihusishwi moja kwa moja na stakabadhi za siri zilizofichuliwa za makaratasi ya kampuni ya Panama.

Lakini baraza hilo kuu la EU lina matumaini kuwa kuwekwa wazi kwa taarifa za kampuni hizo hasa za ulipaji ushuru utapunguza pakubwa ufisadi wa makampuni ya mataifa ya visiwani.