Vyama kumteua waziri mkuu mpya Ukrain

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arseny Yatsenyuk alitangaza kuwa na mipango ya kuondoka ofisini ili kutoa fursa ya kuwepo utulivu nchini humo.

Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ukrain vitajaribu kumteua waziri mkuu mpya baadaye hii leo, huku kukiendelea kushuhudiwa msukosuko wa kisiasa.

Arseny Yatsenyuk alitangaza kuwa na mipango ya kuondoka ofisini ili kutoa fursa ya kuwepo utulivu nchini humo.

Waandishi wa habari wanasema kuwa rais wa Ukrain Petro Poroshenko, yuko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wa nchi hiyo, wakiwemo muungano wa ulaya na marekani pamoja na watu nchi hiyo wanaotaka kuwepo mabadiliko kamili.

Maafisa saba wameondoka serikalini siku za hivi majuzi wakilalamika kuwa serikali haijajitolea kupambana na ufisadi.