Mtu mrefu duniani awasili Mauritius

Image caption Sultan Kösen ana urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51.

Mtu mrefu zaidi duniani raia wa Uturuki Sultan Kösen aliye na urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51 amewasilia nchini Mauritius leo asubuhi.

Sultan alilakiwa na umati katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi, kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye ukusara wa facebook wa mtandao wa habari wa nchi hiyo.

Image caption Aliikinga kitabu Guinness World Records mwaka 2009.

Sultan mara ya kwanza alitajwa kuwa mtu mrefu zaidi duniani mwaka 2009 wakati alitimia urefu wa futi 8 na inchi moja mwaka 2009.

Akiongea wakati aliingia kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness World Records alismea," Singetarajia ningekuwa kwenye kitabu hicho, nikuwa na ndoto lakini bado ulikuwa ni mshangao mkubwa.