Mapigano bado yaendelea Yemen

Haki miliki ya picha
Image caption Zaidi ya watu 6000 wameuwawa kutokana na vita nchini Yemen.

Kumekuwa na mapingano ya hapa na pale nchini Yemen wakati wa siku pili ya kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha vita yanayoongozwa na umoja wa mataifa.

Viongozi wamesema wanajeshi wa Rais Abedrabbo Mansour Hadi, walipambana na wanamgambo wa Houthi katika mkoa wa Marib , karibu na mji unaodhibitiwa na waasi wa Sanaa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi mjini Sanaa

Kwengineko mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejilipua karibu na uwanja wa soka kusini mwa bandari ya Aden na kuwauwa watu wanne.

Watu wengine 10 wamejeruhiwa katika shambulio hilo, ambalo lilikuwa limelenga wanajeshi walioajiriwa.

Zaidi ya watu 6000 wameuwawa kutokana na vita nchini Yemen.