Chibok: Miaka miwili baadaye

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lakini inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?

Miaka miwili iyopita wiki kama hii , wasichana 267 walitekwa nyara kutoka shuleni kwao na wanamgambo wa Boko Haram .

Suala lililolaaniwa vikali kimataifa na kuchochea kampeni ya mitandao ya kijamii iliyojulikana kama #bringbackourgirls na kuweka wazi udhalimu unaotekelezwa na makundi ya uasi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Image caption Shule ya Chibok ilivyobakia sasa

Zaidi ya vijana 200 wa kike hawajapatikana hadi leo .

Katika ripoti hii maalum mwandishi wa BBC Martin Patience alisafiri hadi Chibok kuongea na familia za wasichana na kutembelea shule ambako walitekwa nyara.

Image caption Msitu hapa ni mkubwa .. na ni rahisi sana kwa wanamgambo wa Boko Haram kuvamia msafara wowote wa magari ya kijeshi

Barabara ya kuelekea Chibok imejaa vikwazo na hatari hata hivyo tulisafiri katika msafara wa magari ya kijeshi tukipitia vijiji vilivyotelekezwa .. kimoja baada ya kingine

Taswira

Kile kinachoonekana kama msikiti unaonekana kupigwa risasi kila mahali , Paa lake limeng'olewa ,

Hiki kilikuwa ni kijiji ambacho huenda kilikua ni makaazi ya makumi kadhaa familia , lakini kwa sasa hakuna mtu anayeishi hapa na vichaka vimemea tena kijijini hapa

Msitu hapa ni mkubwa .. na ni rahisi sana kwa wanamgambo wa Boko Haram kuvamia msafara wowote wa magari ya kijeshi

Image caption Msikiti wa Chibok

Saa tatu baadae tuliwasili Chibok mahala kulikokuwa zamani soko maarufu la mji ambao kwa sasa halisikiki.

CHIBOK

Lakini wakati huo Boko Haram walipokuja kuwateka mamia ya wasichana wa eneo hili walibaki na kumbukumbu za kutisha za usiku huo …..

Wazazi hapa wamebakia kusubiri majibu ya wapi waliko watoto wao.

Miongoni mwao ni Mariam Abubakar.

Mwanaye Han Satu alikua na umri wa miaka 17 alipotekwa … alipenda mitindo

Image caption Msafara wa jeshi la Nigeria

''Msichana wangu likua mchapakazi . Alipenda utani na alipenda mavazi.''

''Muda mfupi tu kabla ya kuchukuliwa alikua ameniomba nimnunulie mashine ya kushona nguo''alisema Myrama Abubakar.

Mbele ya nyumba yake ya matope Maryama alivuta nguo alizoacha binti yake .

Alichukua vazi alilolipenda na kuliweka kwenye magoti yake .

Image caption Chibok

''Hii ni gauni aliyotakiwa kuvaa kwenye harusi ya rafiki yake siku moja baada ya kumaliza mitihani .

Lakini mitihani haikufanyika . Nitaitunza gauni hii mpaka atakaporudi alisema mzazi huyo.

Na baade nilizungumza na Binta AbuBakar mama yake Maryam ambaye sasa angekua na miaka 19 -

Image caption Kundi la waandishi wa habari

''Kabla ya kwenda shuleni siku ile alikua anafanya kazi katika duka angu la chakula . Aliweza kufanya mauzo ya dola hamsini! alikua mzuri sana kuwavutia wateja , alikua mfanyabiashara hodari . Hizii ndizo nyakati za mwisho nilizokua naye.

Naomba binti yangu arejee akiwa hai . Lakini kama haitakua hivyo natumai roho yake italala kwa amani . Natumai kumbu kumbu za kutisha alizoziona wakati alipotekwa yatakua ndio mateso yake ya mwisho ,alisema bi AbuBakar.

Haki miliki ya picha
Image caption Mwanaye Han Satu alikua na umri wa miaka 17 alipotekwa … alipenda mitindo

Miaka miwili baadaye hakuna taarifa kuhusu waliko wasichana wa Chibok - Labda wako Chad ama Cameroon - kuna uwezekano mkubwa wengi wao walilazimishwa kuolewa na wapiganaji.

Maisha yanaendelea kurejea taratibu katika hali ya kawaida mjini Chibok na usalama unaimarika.

Lakini inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?