Wakimbizi watoroka kambini DRC

Haki miliki ya picha
Image caption Wakimbizi watoroka kambini DRC

Kambi 5 za wakimbizi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zimesalia mahame baada ya wakimbizi kutoroka vita vilivyozuka katika eneo la Kivu Kaskazini.

Umoja wa mataifa unaoendesha kambi hizo 5 unasema kuwa mapigano yalizuka katika mji wa Mpati na kusababisha zaidi ya wakimbizi 35,000 kutoroka ilikuokoa maisha yao.

UN inahofia usalama wa wakimbizi hao wa ndani kwa ndani.

Image caption Mpati ilikuwa makao ya zaidi ya wakimbizi 35,000

Kwa sasa hakuna njia ya kutathmini hali yao halisi kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo hilo la Kivu kwa takriban mwezi mmoja sasa.

Jeshi la taifa limekuwa likikabiliana na waasi waliojihami.