Ulaya yamshutumu rais wa Macedonia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Gjorge Ivanov

Muungano wa ulaya umelaani hatua ya rais wa Macedonia, Gjorge Ivanov, kuwasamehe wanasiasa waliohusishwa na ufisadi.

Kamishna anayehusika na upanuzi wa muungano huo Johannes Hahn, amesema kuwa msamaha huo hauambatani na uelewa wake wa sheria na hivyo, unahatarisha azma ya Macedonia kuwa mwanachama wa muungano huo.

Taifa hilo limekumbwa na mzozo unaohusiana na madai kwamba chama tawala na wakuu wa idara ya ujasusi , walidukua simu za zaidi ya watu alfu ishirini wakiwemo waandishi wa habari na maafisa wa idara ya mahakama.