Malawi yakumbwa na uhaba wa chakula

Image caption WFP inasema kwa hivi sasa inawasaidia karibu watu milioni tatu nchini Malawi

Rais wa Malawi Peter Mutharika, ametangaza hali ya hatari kutokana na upungufu wa chakula unaosababishwa na hali ya kiangazi kusini mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Shirika la Chakula Duniani WFP limesema kwa hivi sasa linawasaidia karibu watu milioni tatu nchini Malawi kwenye wilaya 23 kati ya 28 zimeathirika sana.

'Upungufu wa mavuno ya mahindi unatarajiwa kushuka kwa asilimia 12 kutoka kwa mavuno ya mwaka jana,' Bwana Mutharika alisema kupitia taarifa yake.

Watu Zaidi watakosa vyakula vya kutosha na watahitaji misaada mwaka huu wa 2016 na 2017.