Mawakala wavamia Mossack Fonseca

Image caption Mossack Fonseca imeshutumiwa kwa kuepuka kulipa kodi na ulaghai.

Mawakala kutoka afisi ya mkuu wa sheria nchini Panama wamevamia jengo la kampuni ya mawakili ya Mossack Fonseca, kutafuta ushahidi wowote unaohusiana na biashara haramu.

Kampuni hiyo imeshutumiwa kwa kuepuka kulipa kodi na ulaghai lakini mwanzilishi wake Ramon Fonseca amesema kuwa operesheni zake zote ni halali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanzilishi wake anasema oparesheni zake ni halali

Wapelelezi kutoka mataifa ishirini na nane wanakutana mjini Paris Ufaransa baadaye kubuni njia ya kimataifa kukabiliana na ukwepaji wa kulipa kodi.

Polisi waliendesha uvamizi huo wakiandama na maafisa kutoka kitengo cha kupambana na uhalifu uliopangwa.

Maafisa walizingira makao hayo huku wakuu wa mashtaka wakiingia kwenye ofisi hizo kufanya uchunguzi.