Nigeria kuongeza sarafu ya Yuan

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sarafu ya Yuan

Nigeria itaongeza sarafu ya China ya yuan katika biashara ya sarafu za kigeni za nchi hiyo kufuatia maafikiano yaliyoafikiwa kati ya serikali hizo mbili.

Kwa sasa karibu asilimia 10 ya sarafu za kigeni nchini Nigeria ni yuan huku zilizosalia zikiwa ni dola za Kimarekania.

Image caption Viongozi wa China na Nigeria

Makubaliano hayo yaliafikiwa wakati wa ziara ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari nchini China, ambapo alifanya mazungumzo na rais Xi Jinping siku ya Jumanne.

Nigeria ambayo ni yenye utajiri mkubwa wa mafuta, ilikuwa ndiyo ya kwanza kutumia sarafu ya yuan barani Afrika kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya kigeni nchini China.