Obama atetea malipo sawa kwa wanawake

Haki miliki ya picha SewallBelmont House
Image caption Makavazi haya ya Sewall-Belmont ni kwa heshima ya wanawake wa Marekani

Rais Barack Obama amezindua makavazi mapya kwa heshima ya kushinikiza usawa wa jinsia hususan malipo sawa kwa wanawake.

Rais Obama mesema makavazi ya Sewall-Belmont na ambayo yaliwahi kuwa makao makuu ya chama cha wanawake yatakua ishara ya kutetea haki za wanawake. Mwaka wa 1916 mwanaharakati Alice Paul alianzisha chama cha wanawake kutetea haki za wanawake katika jamii.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi mwanamke wa Marekani

Makavazi haya yako mjini Washington. Kuzinduliwa kwake kumetokea siku ya kutetea kuwepo malipo sawa.

Siku hii imetengwa kuangazia pengo kubwa kwenye malipo kati ya wanawake na wanaume nchini Marekani.

Malipo ya wastani kwa mwanamke anayefanya kazi rasmi huwa dola 39,621 kwa mwaka ikilinganishwa na mwanamme ambaye hupokea dola 50,383, wote wakiwa wanafanya kazi sawa.