Chibok: Mji uliopoteza wasichana wake

Image caption Hii ni hadithi ya Wasichana watano waliotekwa kutoka shule ya wasichana wa Chibok.

Katika usiku huo ambao Jumai alitekwa kutoka shule ya upili ya wasicha ya Chibok, alimpigia Babake simu.

Alikuwa nyuma ya lori moja lililokuwa linawasafirisha washina hao mateka wa wapihganaji wa kiislamu wa Boko Haram.

Babake alimsihi aruke kutoka kwenye lori hilo lakini kwa bahati mbaya laini ya simu ilikatika.

Daniel, babake, alikimbia kutoka nje ya nyuma kuelekea kwenye sehemu yenye muinuko angalau aweze kupata huduma ya simu kama ilivyokawaida ya vijiji vingi tu barani Afrika.

Simu hiyo ilipopokewa, sauti ya mwanaume ndiyo iliyosikika ikisema ''acha kumpigia mwanao simu ametekwa nyara''

Moyo ulimdundadunda Daniel, alijua kuwa maisha ya mwanaye yamo ''katika mikono ya mwenyezi mungu.'''

Licha ya kuwa wazazi wengine walifurahi kutoa picha za wana wao, Jumai na babake walitulazimu kubadili majina yao kwa hofu ya kujulikana.

Kabla ya kutekwa kwa wasichana wa shule ya Chibok mji huo ulikuwa na wenye utulivu sana.

Image caption Hali halisia katika mji wa Mbalala

Wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram walikuwa wameshambulia miji iliyoko karibu haswa katika maeneo ya Kaskazini.

Daniel ambaye anaishi karibu na mji wa Mbalala alimpeleka mwanaye shuleni iliafanya mtihani wake wa mwisho mnamo tarehe 14 mwezi Aprili mwaka wa 2014.

Hata hivyo usiku huo ndio mji wa Chibok uliposhambuliwa na Jumai akatekwa nyara pamoja na wenzake 275.

Licha ya kuwa mwanaye hakuweza kutoroka kama walivyofanya wasichana wengine Daniel bado ana imani kuwa siku moja atarejea nyumbani.

''Alikuwa anaweza kuendesha baiskeli kama mwanaume''.

Majuzi tu Daniel alimpigia mwanaye simu na sauti ya mwanaume ikajibu ''Hello, hii simu ni ya mke wangu je nikusaidie vipi ?

Image caption Hansatu Abubaker

Daniel akamuuliza ''na wewe ni nani ?

Yule mwanaume naye akamuuliza ''yeye ni nani'' na akakata simu.

Baadaye Daniele alipiga simu hiyo tena na mara hii akadanganya kuwa anampigia simu kutoka maiduguri. mji mkuu wa jimbo la Borno.

Alijiita Amir Abdullahi - na akasema kuwa yeye ndiye kiongozi wa waasi.

akamuambia iwapo anamjua basi hangelipiga simu hiyo.

Mbalala yasalia mahame
Image caption Maryam Abubakar

Jumai anatokea Mbalala takriban kilomita 11 kutoka Chibok.

Kati ya wale wasichana waliotekwa 25 wanatokea Mbalala

Kitambo mji huo ulikuwa maarufu sana na wafanyibiashara wa mifugo kutoka Kano, lakini hivi sasa vibanda vyote vimesalia tupu.

kwa sasa jeshi huthibiti kila kitu wanachokifanya huko kwa mfano huwezi kununua chakula kwa wingi.

Ukiwa na jenerata huaruhusiwi kuiwasha usiku.

Ukirejea nyumbani unakumbana na giza totoro.

Eneo letu halina umeme kazi kwa vijana shule wala hospitali.

Vijana wengi wa eneo hilo wanahamia kwengineko kutafuta ajira, Wasichana kwa upande wao wanaolewa mapema iwezekanavyo.

Wanawake wa huko wanajishughulisha na biashara ya kuuza kaimati na bidhaa zingine za mapishi.

Akiwa likizoni Maryam Abubaker alikuwa akimsaidia mamake na mapishi ya keki ya maharagwe kaimati na bidhaa zingine .

Siku hiyo aliyotekwa Maryam alikuwa amemsaidia kuuza katika duka lake siku hiyo mamake anasema kuwa ''alifaulu kupata dola $50''

''Alikuwa ni mfanyibiashara maarufu.

Image caption Grace Paul

''Alikuwa ni mvivu sana shambani lakini ukimpa fursa ya kuuza ,alikuwa mweledi wa kuwashawishi wateja kununua ''anasema mamake akikumbuka dakika za mwisho alipokuwa na binti yake.

Rafiki wa Maryam wa karibu alikuwa na dadake wa kambo Hansatu.

Walikuwa wanashona nguo zinazofanana na walikuwa na marafiki walewale.

Hansatu alikuwa ni mwanamitindo mbunifu na alikuwa amemsihi mamake amnunulie mashine ya kushona nguo.

Baada ya kutekwa ndugu zake wadogo walikuwa wanauliza kwanini harudi nyumbani.

Kila walipoona nguo zake walimuuliza aliko hadi ikamlazimu mamake kuzitoa zote na kuzifungia sehemu moja anagalau azime maswali hayo.

Anatuonesha nguo maalum aliyokuwa amepangia kuivaa akienda harusini.

''nitaziweka hadi pale atakaporudi'' anasema mamake huku akilengwa na machozi.

Hansatu Abubaker

Hizi ni baadhi ya vitu ambavyo wazazi wa wasichana waliotekwa wamesalia navyo tu kwa tumaini la siku moja kuwaona tena wana wao.

Tangu watekwe wasichana hao, serikali haijawahi kusema waliko.

Serikali ya wakati huo ilikataa katakata kuhusiana na wazazi najambo lililosababisha hasira kubwa na wao kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Serikali hii mpya ambayo iliahidi kutokomeza kabisa swala la ugaidi haijafanya lolote kwa nia ya kuwapata wasichana hao.

Ukweli ni kwamba hakuna ajuaye waliko.

Kwa familia nyingine hii picha ndiyo kumbukumbu tu walionayo kwa sasa.

Image caption Aisha Greman

Tangu kutekwa nyara kwa watoto hao hawajakuwa na habari yeyote kumhusu.

Grace Paul

Grace angekuwa anatimiza miaka 19 sasa.

Alikuwa muimbaji hodari anasema babake.

Alipenda sana hisabati na alitaka kuwa daktari.

Picha hiyo ya pekee waliosalia nayo wamempa jirani yao iliaipige chapa.

Wasichana hao wa Chibok waliotekwa ndio wale waliokuwa na ndoto si haba kijijini humo.

Hii ni kwa sababu takwimu zinaonesha kuwa nusu ya vijana nchini Nigeria huwa hawamalizi masomo ya shule ya upili.

Kwa hivyo hao ni baadhi ya wachache waliokuwa na nia ya kuendeleza maisha yao kupitia kwa masomo.

Aisha Greman alikuwa na umri wa miaka 17 alipotekwa nyara.

Aisha Greman
Image caption Jinkai Yama

Alisusia ndoa akiwa bado yuko shuleni babake anasema.

Alikuwa ni mchapa kazi shupavu na alikusudia kupata shahada ya utabibu.

Jinkai Yama alikuwa kifungua mimba katika familia yenye wasichana wanne.

Alitaka sana kujiunga na jeshi la taifa, na hata alikuwa akishiriki katika mipango ya huduma ya vijana mtaani kwao.

Dada zake wanamuulizia sana .

Mwezi uliopita kunamsichana aliyedai kuwa yeye ni miongoni mwa wasichana wa Chibok alipokamatwa na maafisa wa usalama baada ya bomu aliyokuwa amebeba kukosa kulipuka.

Maafisa wa Cameroon waliwahitaji wazazi kwenda kuthibitisha madai yake.

Kwa bahati mbaya alikuwa siye, alikuwa anatokea Bama mji ulioko kaskazini ya Chibok.

Kila inaponyesha mvua, babake Jinkai huwa anafunga macho na kupiga picha akitaka kujua mwanaye aliko anakaaje yuala nini analala wapi na mambo mengine kama hayo

Kama wazazi wenza ameanza kupoteza matumaini ya kumuona bintiye akiwa hai.

Hana imani kuwa serikali inafanya jambo lolote kuwapata wakiwa hai wanawao.

Jinkai Yama

Hawaamini kabisa iwapo serikali inakusudia kwa njia yeyote kuwanusuru.

Kuna madai ya njama nyingi mno.

Babake Jumai Daniel, anaamini iwapo serikali ilikuwa na nia ya kuwapata mabinti hao, wangelitumia namba ya simu ya binti yake kujua waliko!

Amekataa kuwapa nambari hiyo kwa kuwa haamini iwapo watamfaa.

Image caption Jeshi la Nigeria

Jeshi la taifa pia haliendi Mbalala, ila kila jumapili wanakwenda huko kuwafukuza wafanyibiashara kutoka sokoni.

Wanahofia kuwa endapo kutakuwa na mkusanyiko wa watu huenda wakashambuliwa na walipuaji wa kujitolea muhanga.

Walipokuja Chibok wanajeshi waliwaonya kuwa mtu yeyote anaweza kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga.

Kwa hilo walimaanisha hata wasichana.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wasichana wengi ndio wamekuwa wakijilipua na kusababisha maafa mengi.

Wameshambulia masoko na hata kambi za wakimbizi.

Mwezi februari mshambuliaji wa kujitolea muhanga aliwaua watu 13 katika soko moja la Chibok.

Mama mmoja ambaye mwanaye alitekwa nyara na Boko Haram anapinga dhana hiyo.

''Mimi nilimzaa binti yangu kama vile nilivyowazaa wengine na nilimlea ipasavyo, hawezi kuwa muuaji.

"hata kama atakuja nyumbani akiwa amejihami na bunduki, acha tu aniue mimi ila nitamkaribisha nyumbani ''

Boko Haram

Kundi hili la wanamgambo wa kiislamu wanaopinga elimu kutoka Magharibi lilianzishwa mwaka wa 2002.

Lengo lao kuu ilikuwa kupimnga masomo ya kisasa wanayoita ''elimu ya dunia''

Image caption Mzazi wake Binti abubaker

Jina Boko Haram linamaanisha ''elimu ya magharibi ni haramu'' katika lugha ya Hausa.

Boko haram ilianza kampaeini ya kijeshi mwaka wa 2009.

Maelfu ya watu wameuawa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria na maelfu zaidi wametekwa nyara wakiwemo takriban wasichana 200 wa Chibok.

Waliapa utiifu kwa kundi la kiislamu la Islamic State na kujiita ''Tawi la Magharibi mwa Afrika''

Waliteka maeneo makubwa mno ya Kaskazini mwa Nigeria na wakajitangazia himaya yao

Himaya yao imekombolewa zaidi na wanajeshi wa muungano wa mataifa ya Afrika Magharibi