China yaonyesha picha za raia wa Taiwan

Image caption Raia wa Taiwan wakiwasili China

Vyombo vya habari vya serikali nchini China, vimeonyesha picha za raia wa Taiwan waliofukuzwa kutoka nchini Kenya kwenda China, waliposhukiwa kuhusika kwenye ulaghai wakiwa chini ya kuzuizi cha polisi.

Hi ndio taarifa ya hivi punde inayowahusu raia 45 wa Taiwan, wanaokisiwa kuhusika kwenyr ulaghai wa simu, waliasafirishw kwenda nchini China wiki hii.

Taiwan imesema imeishtaki Kenya kwa kupuuza uamuzi wa mahakama, uliwaondolea mashtaka baadhi wa washukiwa na kushirikiana na China kawasafirisha watu hao kinyume na sheria.