Jamhuri ya Czech kubadilisha jina

Image caption Jamhuri ya Czech kubadilisha jina

Jamhuri ya Czech ina mipango ya kubadilisha jina lake na kuitwa "Czechia" ili kufanya rahisi kwa makampuni na timu za spoti kutumia jina hilo kwa bidhaa na mavazi.

Nchi hiyo itasalia na jina lote lakini Czechia litakuwa jina rasmi fupi sawa na Ufaransa amabyo ni Jamhuri ya Ufaransa.

Ikiwa litaidhinishwa na bunge jina hilo litawasilishwa kwa Umoja wa Mataifa.

Image caption Jamhuri ya Czech ni maarufu kwa mchezo wa magongo

Jamhuri ya Czech ilibuniwa wakati Czechoslovakia iligawanyika mara mbuli mwaka 1993.

Moja ya bidhaa maarufu za nchi hiyo ni pamoja na Bia ya Pilsner na timu ya magono ambayo wa sasa hutumia jina Czech.

Hata hivyo wakosoaji wanasema kuwa jina "Czechia" ni mbaya na linafanana na jina Chechnya.