Tetemeko la ardhi laua 9 Kumamoto, Japan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uharibifu wa tetemeko la ardhi nchini Japan

Takriban watu tisa wameuwa wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo la kusini mwa Japan siku ya Alhamisi.

Tetemeko hilo lilitokea karibu na jiji la Kumamoto katika kisiwa cha Kyushu, kilomita 1,300 kusini magharibi mwa Tokyo.

Wengi wa waathiriwa ni kutoka mji wa Mashiki ambapo jengo moja liliporomoka na pia nyumba nyingi kuharibiwa.

Kote nchini humo, zaidi ya watu 40,000 waliondoka manyumbani mwao lakini baadhi yao wameanza kurudi licha ya kuwepo mitetemeko midogo midogo.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kwa serikali imetuma polisi, wazema moto na wanajeshi kuendesha oparesheni za uokoaji.