Pembe za Ndovu kuchomwa Kenya

Image caption Pembe zitateketezwa tarehe 30 mwezi huu

Malori yaliyosheheni Pembe za Ndovu yamewasili kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi kutoka kote nchini .

Takriban tani 105 za Pembe za Ndovu zitateketezwa moto tarehe 30 mwezi huu wa Aprili kwa mujibu wa shirika la AFP.

Mwezi Januari AFP ilisema kuwa wasanii wa Hollywood Leonardo DiCaprio na Nicole Kidman watahuia shughli hiyo ya kuchoma pembe hizo.

Picha za kuchomwa kwa Pembe za Ndovu zimekuwa zikionekana nchini kenya, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa itachukua hadi wiki moja kuchoma kabisa pembe moja ya ndovu.