Mugesera afungwa jela maisha Rwanda

Musegera Haki miliki ya picha AFP
Image caption Musegera alitorokea Canada baada ya mauaji kutokea

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Leon Mugesera amefungwa jela maisha na mahakama kuu nchini Rwanda, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Mugesera anadaiwa kutoa matamshi ya kuchochea chuki dhidi ya Watutsi mwaka 1992.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times la Rwanda, Mugesera anadaiwa kusema Watutsi wanafaa kurejeshwa Ethiopia kwa kuuawa au kutupwa kwenye mito.

Alisema hayo akitoa hotuba 1992 wakati huo bado akiwa mwanachama wa chama kilichokuwa kinatawala wakati huo cha MRND.

Alitorokea Canada baada ya mauaji ya kimbari kutokea lakini akarejeshwa Rwanda mwaka 2012 baada ya juhudi za miaka mingi za kuzuia hatua hiyo katika mahakama za Canada.

Alishtakiwa makosa ya kuchochea mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.