Kerry:Tungedungua ndege za Urusi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meli ya jeshi la Marekani

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekania John Kerry, amesema kuwa jeshi la wanamaji la nchi hiyo lilikuwa na haki ya kudungua ndege za urusi, zilizoruka karibu na meli ya jeshi la marekani katika bahari ya Baltic.

Kamanda wa meli hiyo ya USS Donald Cook, alisema kuwa ndege za jeshi la Urusi zilikaribia chombo chake siku ya Jumatatu.

Bwana kerry amezitaja hauatua hizo kama uchokozi na hatari. Amesema kuwa marekani haiwezi kudhulumiwa baharini.

Waziri wa ulinzi nchini Urusi kwa upande wake amesema kuwa meli hiyo ya Marekani ilipita karibu na kambi ya jeshi la wanamaji wa Urusi na ndege zake zilifuata sheria.