Rosberg ashinda mbio za magari China

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rosberg ashinda mbio za magari China

Dereva wa mbio za magari ya langa langa wa timu ya Mercedes , Nico Rosberg,ameshinda mbio za langalanga za Chinese Grand Prix.

Ushindi huo wamaanisha , mjerumani huyo ameshinda mashindani yote matatu ya msimu huu kwani alishinda yale ya Australia na Bahrain.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ushindi huo wamaanisha , mjerumani huyo ameshinda mashindani yote matatu ya msimu huu

Mpinzani wake mkuu ambaye ndiye dereva bingwa mtetezi Lewis Hamilton aliyeanza mashindano hayo akiwa katika nafasi ya mwisho alijifurukuta na kumaliza katika nafasi ya 7.

Raia huyo wa Uingereza alipata ajali na akalazimika kusimama takriban mara 5 ilikurekebisha gari lake.

Kutokana na ushindi huo Hamilton sasa ana mlima wa kupanda ilikujaribu kuziba pengo la alama 36 katika mashindano 18 yaliyosalia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kutokana na ushindi huo Hamilton sasa ana mlima wa kupanda ilikujaribu kuziba pengo la alama 36 katika mashindano 18 yaliyosalia.

Dereva wa Ferrari, Sebastian Vettel, alibahatika na kumaliza katika nafasi ya pili licha ya kukumbwa na ajali mbaya dhidi ya mwendesha mwenza wa Ferrari Kimi Raikkonen katika mzunguko mmoja.