Maandamano: Marekani yaikosoa Gambia

Haki miliki ya picha AFO
Image caption Marekani yaikosoa Gambia

Marekani imelaani, kile ilichoeleza kuwa hatua kali zilizochukuliwa na serikali ya Gambia, kupambana na maandamano ya amani yaliyofanyika huko.

Waandamanaji walikamatwa Alhamisi na jana.

Waziri wa habari wa Gambia, Sheriff Bojang , alisema wale waliokamatwa, waliandamana kinyume cha sheria.

Kati yao alikuwa kiongozi wa upinzani, Ousainou Darboe.

Taarifa ya Marekani, haikutaja kifo cha mwanasiasa mwengine wa upinzani, Solo Sandeng, kinachosemekana kutokea gerezani ambacho kilizusha maandamano ya jana.

Waziri huyo wa Gambia, aliiambia BBC, kwamba hawezi kuthibitisha kama Bwana Sandeng amefariki au la.