Boko Haram wavamia kambi ya jeshi Nigeria

Haki miliki ya picha
Image caption Boko Haram wavamia kambi ya jeshi Nigeria na kuua wanajeshi

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wameishambulia kambi ya jeshi la Nigeria mapema asubuhi ya leo na kuua idadi kubwa ya wanajeshi huko Borno.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Idadi kamili ya waliouawa haijajulikana.

Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na mapema wakiwa wamelala.''

''Wapiganaji hao walikuwa wamejihami kwa silaha kali na kusababisha maafa makubwa upande wa wanajeshi''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui hata ni wangapi waliojeruhiwa'' alisema mwanajeshi huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake

Kambi hiyo ndogo iliyoko katika kijiji cha Kareto ilikuwa na wanajeshi wachache ambao kazi yao ilikuwa ni kulinda ngome kabla ya kikosi kikubwa zaidi kuwasili.

Hata hivyo mwanajeshi huyo anasema kuwa idadi ya wapiganaji hao ilikuwa kubwa mno hata wanajeshi kadhaa walitoroka ilikuokoa maisha yao.

''Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na mapema wakiwa wamelala.''

''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui hata ni wangapi waliojeruhiwa''

''Baadhi yetu walitoroka maji yalipozidi unga''

''Tuligundua idadi ya wavamizi ilikuwa ni kubwa kuliko yetu'' mwanajeshi mwengine aliiambia shirika la habari la AFP.

Haki miliki ya picha Boko Haram Twitter
Image caption ''Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.

Wapiganaji kadhaa waliuawa katika makabiliano hayo yaliyodumu kwa saa kadhaa kulingana na wenyeji wa kijiji hicho.

Hata hivyo jeshi lilijitahidi na kuikomboa kambi hiyo baada ya mashambulizi ya angani kuwasili na kuwaokoa wanajeshi walikuwa wamesakamwa ardhini.

Idadi kamili ya waliouawa haijajulikana.