UN: Burundi inawatesa wapinzani wake

Haki miliki ya picha
Image caption Idadi ya watu wanaoteswa nchini Burundi imeongezeka maradufu.

Idadi ya watu wanaoteswa nchini Burundi imeongezeka maradufu.

Umoja wa mataifa unasema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza mwaka huu takriban watu 400 wameripotiwa kukamatwa na vyombo vya dola na kisha kuteswa..

Image caption Zeid Ra'ad Al Hussein anasema kuwa mawakala wake wamerekodi visa 345 za mateso na dhulma dhidi ya watu wanaokisiwa kuwa wapinzani nchini Burundi.

Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu wa Umoja huo wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein anasema kuwa mawakala wake wamerekodi visa 345 za mateso na dhulma dhidi ya watu wanaokisiwa kuwa wapinzani nchini Burundi.

Tangu machafuko ya kisiasa yalipoanza mwaka mmoja uliopita, takriban watu 600 wameshikwqa na kuteswa na vyombo vya serikali ya rais Pierre Nkurunziza.

Haki miliki ya picha
Image caption Machafuko yalianza nchini Burundi rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wake wa tatu .

''Hao ndio waliokuwa na shime ya kujitokeza ,tunashuku kuwa idadi ya wale walioteswa ni kubwa mno ila kutokana na hofu ya kukabiliwa na maafisa wa usalama wengi wanajificha'' alisema afisa huyo wa UN.

Wale wanaokamatwa na kuteswa mara nyingi wanasema kuwa wanapitia dhulma hiyo ndani ya vituo vya idara ya usalama wa taifa na kijasusi ya Burundi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hadi kufikia sasa takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki

Machafuko yalianza nchini Burundi rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wake wa tatu .

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Pierre Nkurunziza

Wapinzani wake walimkashifu kwa kukiuka katiba ya taifa huku rais mwenyewe akisisitiza kuwa wala hakukiuka kamwe katiba kwani muhula wa kwanza , alipoongoza taifa hilo hakuchaguliwa na umma bali wajumbe wa kamati maalum ya upatanisho iliyoundwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe 2005.

Hadi kufikia sasa takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki huku zaidi ya watu laki mbili u nusu wakilazimika kutorokea mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mapigano mapya.