Wahamiaji wa Afrika Mashariki wafa maji

Haki miliki ya picha AFP

Kikundi cha wahamiaji zaidi ya arobaini kutoka Afrika mashariki wameokolewa wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranian huku ikisemekana kuwa mamia ya watu waliokuwa pamoja nao walizama usiku wa manane , kwa kushindwa kuhimili uzito iliyoubeba.

Wahanga hao awali walishikiliwa nchini Ugiriki ,waliiambia BBC kuwa watu mia mbili kati yao walisalia nchini Libya na kusema kuwa wakati wako baharini wasafirishaji haramu wa binadamu waliwaambia wahamie katika boti ingine ambayo ilikuwa tayari imejaa wahamiaji wapatao mia tatu.

Hata hivyo maafisa wanaohusika na usafirishaji majini, hawaja thibitisha tukio hilo nalo shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi limeandika katika ukurasa wake wa kijamii wa Tweeter kuwa taarifa hiyo haiko sahihi.