Majanga yasababisha hasara kubwa duniani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto wa msituni

Majanga ya kiasili kote duniani yamesababisha hasara za kiuchumi za karibu dola trillioni 7 tangu mwaka 1900 kwa mujibu wa hesabu zilizofanywa na wanasayansi.

Takwimu ambazo zina takriban visa 35,000 zinaonyesha kuwa majanga hayo pia yamesababisha vifo vya watu milioni 8.

Udadisi huo unastahili kuzisaidia serikali kujiandaa kwa majanga na hatua ambazo zitachukua, kwa mujibu wa watafiti.

Haki miliki ya picha
Image caption Gharika ya tsunami

Kundi hilo la wanasayansi lililoongozwa na taasisi moja ya teknolojia nchini Ujerumani, lilitafuta taarifa kutoka kwa vyombo vya habari na kumbumbu za kale kwa habari zote lingeweza kupata kuhusu mafuriko, kiangazi, gharika, volkano , mitetemeko ya ardhi na moto wa msituni.

Kati ya mwaka 1900 na 2015 takribana asilimia 40 ya hasara ilitokana na mafuriko asiliamia 12 ilitokana na kiangazi asilimia 2 kutoka kwa moto wa msituni na asilimia moja ilitokana wa volkano.