Riek Machar asubiriwa kuwasili Juba

Image caption Walinzi kwenye uwanja wa ndege wa Juba

Kuna hali ya sintofahamu katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, wakati watu wanasubiri kuwasili kwa kiongozi wa waasi Riek Machar.

Anatarajiwa kuchukua wadhifa wa makamu wa rais kwenye serikali mpya ya umoja wa kitaifa ambayo ni hatua kubwa katika kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Bwana Machar alitarajiwa kuwasili wakati kama huo jana, lakini akaairisha safari yake kutokana na matatizo ya usafiri kulingana na msemaji wake.