Marekani kutuma wanajeshi 200 Iraq

Haki miliki ya picha AP
Image caption Idadi ya wanajeshi wa Marekani walio Iraq itafikia 4100

Marekani itapeleka wanajeshi 200 zaidi nchini Iraq kusaidia katika vita dhidi ya kundi la Islamic State

Hatua hiyo itasababisha idadi ya wanajeshi wa Marekani walio nchini Iraq kufikia karibu 4,100.

Kando na wanajeshi hao, ndege za helicopter aina ya Apache nazo zitapelekwa kwa mara ya kwanza kupambana na Islamic state nchini Iraq.

Image caption Ndege ya Helkopta aina ya Apache

Waziri wa ulinzi nchini marekani Ash Carter alitoa tangazo hilo wakati alifaya ziara ambayo haikutangazwa mjini Baghdad, ambapo alikutana na maafisa wa kijeshi wa Marekana na waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi.

Marekani pia ina mipango wa kuvipa vikosi vya Peshmerga ambavyo vinapigana na Islamic State zaidi ya dola milioni 400 kama msaada.