Idadi ya waliokufa Ecuador yazidi 500

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Takriban watu 2000 hawajulikani waliko

Serikali nchini Ecuador inasema kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye tetemeko kubwa la ardhi la siku ya Jumamosi, imeongezeka hadi zaidi ya watu 500.

Naibu waziri wa mambo ya ndani (Diego Fuentes) ameonya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka zaidi kwa sababu waokoaji wanazidi kukosa matumaini ya kupata manusura zaidi.

Takriban watu 2000 bado hawajulikani waliko. Watu 20,000 wameachwa bila makao kufuatia tetemeko hilo la uzito wa 7.8 katika vipimo vya richa lililoikumba nchi hiyo.