Esperance yaizamisha Azam

Image caption Esperance yaizamisha Azam.

Klabu ya soka ya Azam FC imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora kwenye mechi iliyoandaliwa mjiniTunis, Tunisia.

Matokeo hayo yanafanya Azam FC inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, itolewe kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya awali kushinda 2-1 mjini Dar es Salaam.

Mabao ya Esperance yalifungwa na wachezaji Saad Bguir dakika ya 47 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 19, Dakika ya 63.

Haithem Jouini alifunga kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aishi Manula kufuatia krosi ya Hoiucine Regued na dakika ya 80, Fakhreddine Ben Youssef akafunga la tatu akimalizia pasi ya kiungo Driss Mhirsi.