Ethiopia yaomboleza vifo vya raia wake

Haki miliki ya picha
Image caption Zaidi ya watu 200 waliuawa eneo la Gumbella nchini Ethiopia.

Ethiopia imetangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa zaidi ya watu 200 waliauawa wakati kulitokea uvamizi mbaya kwenye mbaya katika eno lililo magharibi la Gambella.

Bendera kote nchini humo na kwenye balozi zote za Ethiopia katikja nchi za ng'ambo zinapepea nusu mlingoti.

Image caption Wavamizi hao ni kutoka kabila la Murle la nchini jirani ya Sudan Kusini.

Rambirambi zimekuwa zikitumwa kutoka nchi tofauti na mashirika ya kimataifa ambayo yamelaani mauaji hayo, na kutekwa nyara kwa zaid ya watoto 108 wakati wa shambulizi hilo lililoendeshwa na watu waliokuw wamejihamia vikali kutoka kabila la Murle la nchini jirani ya Sudan Kusini.

Jeshi la Ethiopia linasema kwa linawatafuta watu hao ili kuwakoa watoto waliotekwa. Akihutubia taifa, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, alisema kuwa washambuliaji 60 wameuawa katika jitihada zinazoendelea za uokoaji, na kwamba serikali yake inashirikiana na serikali ya Sudan Kusini.