Kanye West ashtakiwa kwa madai ya ulaghai

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kanye West na mkewe

Shabiki mmoja ameamua kumshtaki nyota wa muziki wa Rap Kanye West pamoja na huduma ya muziki ya Tidal kuhusu kutolewa kwa albamu mpya ya mwanamuziki huyo,The life of Pablo.

Justin Baker-Rhett anadai alidanganywa kutia saini na kujiunga na huduma hiyo ya moja kwa moja,kwa kuwa ilikuwa njia ya pekee ya kununua albamu hiyo ya West.

Alisema kuwa alijiunga na Tidal baada ya mwanamuziki huyo kusema kuwa albamu yake haitauzwa mahali pengine.

Na sasa anasema kuwa hatua hiyo ni ya kilaghai na ililenga kuipatia Tidal mamilioni ya wateja.

Kanye West alitoa albamu yake mwezi mmoja baadaye katika Apple Muzic,Spotify pamoja na katika mtandao wake.

Baker Rhet anasema kuwa hatua hiyo iliiongezea wateja Tidal mara tatu na kupiga jeki thamani yake kufikia dola milioni 84.