Newcastle watoka sare ya 1-1 na Man City

Newcastle walifaniniwa kutoka sare ya bao moja na Manchester City licha ya bao la sergio Aguero kutiliwa shaka.

Aguero tayari alikuwa ameotea wakati alipata kiki safi kutoka kwa Aleksandar Kolarov na bila kusita akatikiza wavu wa Newcastle.

Hata hivyo Vurnon Anita alifanya mambao kuwa sawa baadaye.

Kipa ya Man City Joe Hat alijikakamua kuzima kitisho cha Georginio Wijnaldum, na kuhakikisa kuwa Newcasle imesalia chini ya jedwali nyuma na Sunderland na Norwich.

Jitihada hizo za kipa wa timu ya England, ziliwanyika wenyeji pointi muhimu ambazo zingewainua katika jedwali.