Malkia Elizabeth atimiza 90

Haki miliki ya picha PA

Malkia Elizabeth ametimiza miaka tisini ya kuzaliwa. Malkia atasheherekea siku hii kwa kukutana na wananchi wake katika matembezi atayafanya huko Windsor.

Malkia Elizabeth ametawala kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza, muda unaokadiriwa kufikia zaidi ya sitini na nne.

Ndiye kiongozi wa kifalme Uingereza aliyeongoza muda mrefu zaidi. Amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 68 na matembelea nchi 117 duniani. Amefanya kazi na Mawaziri Wakuu 12 Uingereza.