Somalia yazuia raia wake kwenda Sudan

Image caption Somalia inatazamia kuwazuia vijana ambao hufanya safari hatari kwenda Ulaya

Somalia imewaambia raia wake kuwa hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchini Sudan, ambacho ni kituo maarufu kwa wahamiaji wanaosafiri kwenda Ulaya kinyume na sheria.

Afisa mkuu wa uhamiaji Abdullahi Gafow, alisema kuwa wasomali ambao wataruhusiwa kusafiri kwenda Sudan ni wale wanaohusika na masuala ya kidiplomasia.

Bwana Gafow alisema kuwa anatazamia kuwazuia vijana wa kisomali ambao hufanya safari hatari kwenda Ulaya.

Mamia ya wahamiaji wengi wao rais wa Somalia, wanaripotiwa kufa maji mapema wiki hii wakati mashua yao ilizama katika bahari ya Mediterranean.