Ethiopia yatekeleza operesheni Sudan Kusini

Image caption ramani ya mpaka wa Sudan Kusini na Ethiopia

Serikali ya Ethiopia inasema kuwa wanajeshi wake wamelizingira eneo moja nchini Sudan Kusini ambapo inaamini zaidi ya watoto 100 waliotekwa nyara wanazuiliwa.

Watoto hao walitekwa katika uvamizi wa mpakani ijumaa iliopita,ambapo zaidi ya watu 200 waliuawa.

Image caption Wanajeshi wa Ethiopia

Ethiopia imesema kuwa itawavamia washambuliaji wanaodaiwa kutoka katika jamii ya Murle.

Washambuliaji hao wanadaiwa kuingia nchini Ethiopia kutoka Sudan Kusini na kuchukua mifugo na mara nyengine huwateka watoto.