Zuma: Uchunguzi haukunipata na makosa

Image caption Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amesema uchunguzi ulioanzishwa miaka mitano iliyopita, kuchunguza ununuzi wa silaha uliogharimu taifa hilo dola bilioni tano, umebainisha kuwa hakuna ushahidi wowote wa ufisadi au ulaghai.

Tume hiyo iliundwa kuchunguza mkataba huo uliosainiwa miaka ya tisini, kufuatia madai ya ufisadi, wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, helikopter na meli za kivita.

Tume hiyo sasa imesema kuwa hakuna ushahidi wowote kuthibitisha kuwa maamuzi wakati wa kusaini mkataba huo, yalichukuliwa baada ya maafisa waliohusika kuhongwa.