Idriss Deby ashinda uchaguzi wa urais Chad

Idris Haki miliki ya picha AFP
Image caption Deby ameongoza Chad tangu 1990

Rais wa Chad Idriss Deby ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika wiki mbili zilizopita.

Kiongozi huyo alipata asilimia 60 ya kura zilizopigwa uchaguzini tarehe 10 Aprili.

Amekuwa madarakani tangu 1990 alipoingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo alimaliza wa pili akiwa na asilimia 13 ya kura.

Upinzani ulikuwa umetilia shaka uchaguzi huo.

Chad ni mwenyeji wa kikosi cha mataifa matano ambayo yamechangia majeshi yanayopigana na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram kutoka Nigeria.