Machar awekewa masharti ya kuingia Juba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Salva Kiir

Sudan Kusini inasema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar hawezi kwenda mji mkuu Juba hii leo.

Waziri wa habari alisema kuwa serikali itatoa tu kibali kwa ndege itakayombeba Machar baada ya waangalizi kubaini kiasi cha silaha wafanyikazi wake watakuwa nacho.

Machar kwa sasa yuko nchini Ethiopia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Riek Machar

Siku ya Ijumaa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon alitoa wito kwa Machar kurejea nchini Sudan Kusini bila kuchelewa