Banki Moon amtaka Machar kurejea Juba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Riek Machar

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametoa wito kwa kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar kurejea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Juba bila kuchelewa.

Bwana Machar alikuwa anatarajwa kurejea Juba siku ya Jumatatu kama sehemu ya makubaliano yaliyoafikiwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili.

Lakini alichelewesha tena kurejea kwake kutokana na tofauti kuhusu ni jeshi kiasi gani na silaha zipi angebeba.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Riek Machar na Salva Kiir

Akiwa mjini Juba anatarajiwa tena kuchukua wadhifa wa makamu wa rais lakini wakati huu ndani ya serikali ya mpito ya muungano wa kitaifa.